Ifakara Health Institute (IHI) – au kwa kifupi Ifakara – ni taasisi inayoongoza katika utafiti wa afya barani Afrika, ikiwa na rekodi nzuri ya kuendeleza, kujaribu na kuthibitisha uvumbuzi kwa ajili ya afya. Tunaongozwa na majukumu ya kimkakati ya msingi ya utafiti, mafunzo na huduma. Ifakara inajumuisha fani mbalimbali za kisayansi, kuanzia sayansi ya kimsingi ya kibaolojia na ikolojia hadi majaribio ya kitabibu, utafiti wa mifumo ya afya, tafsiri ya sera na utekelezaji wa programu za afya...