Mtaala huu wa kilimo ni toleo lililorekebishwa linalochukua mahali pa mtaala wa mwaka 1997. Mchakato wa marekebisho umelenga kwenye mabadiliko ya mtazamo kutoka kwenye Mtaala wa Maudhui hadi Mtaala wa Ujuzi. Aidha, umeshamiria kuzingatia mabadiliko ya kijamii, kisiasa, kitamaduni, kiuchumi, ya kimataifa, ya kiteknolojia na masuala ya kijamii yanayovuka mipaka. Mada nyingine katika mtaala wa zamani zimebadilishwa na mada mpya.
Mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji kwa kutumia mtaala huu...