Hii hapa Majina 418 ya Walioitwa Kuanza Uzalishaji Programu ya BBT Wizara ya Kilimo inawatangazia vijana 418 waliopangiwa shamba la Mlazo/Ndogowe kwamba wanapaswa kuwasili shambani kwa ajili ya kuanza uzalishaji katika msimu huu wa kilimo.
Tafadhali zingatieni muda na kufuata utaratibu uliopangwa.
Wizara ya Kilimo inawasisitiza vijana kufuata maelekezo haya na kuhakikisha wanazingatia ratiba.
Ratiba ya Kuwasili
Utaratibu wa kuwasili umegawanywa katika makundi mawili:- Kundi la Kwanza: Vijana 209 wataripoti tarehe 12 Januari 2025.
- Kundi la Pili: Vijana 209 wataripoti tarehe 13 Januari 2025.
Eneo la Mapokezi
Vijana wote wanapaswa kufika katika Ofisi ya Wizara ya Kilimo - Kilimo IV Dodoma kwa ajili ya usajili, uhakiki, na kukamilisha taratibu muhimu.- Mapokezi yatafanyika kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 6:30 mchana.
- Usafiri kuelekea shambani Mlazo/Ndogowe utatolewa, na mabasi yataondoka saa 7:00 mchana kila siku.
Tafadhali zingatieni muda na kufuata utaratibu uliopangwa.
Masharti ya Programu
- Makazi: Serikali itatoa makazi kwa mnufaika pekee bila mtegemezi.
- Gharama Binafsi: Kila kijana atawajibika kujigharamia mahitaji binafsi wakati wote wa kushiriki programu.
- Kuzingatia Mwongozo: Washiriki wanatakiwa kufuata taratibu za Programu kwa mujibu wa Mwongozo Na. 1 wa 2023: Utoaji Mafunzo Katika Vituo Atamizi na Uendeshaji wa Mashamba Makubwa ya Pamoja ya BBT (BBT Block Farms).
Tarehe za Mwisho za Kuwasili
- Kuanzia tarehe 14 Januari 2025, vijana watakaochelewa wanapaswa kuripoti moja kwa moja shambani Mlazo/Ndogowe.
- Ifikapo tarehe 30 Januari 2025 saa 8:00 mchana, zoezi la kupokea vijana litafungwa rasmi.
Wizara ya Kilimo inawasisitiza vijana kufuata maelekezo haya na kuhakikisha wanazingatia ratiba.
Ajira
TAARIFA KUHUSU USAILI WA KADA ZA UALIMU 2024/2025 AJIRA PORTAL - UTUMISHI AJIRA ZA WALIMU 2025
Ajira za Ualimu 2025