What's new
Majina ya Walioitwa Kazini Sekretarieti ya Ajira Utumishi | Taasisi Mbalimbali PDF

Ajira Majina ya Walioitwa Kazini Sekretarieti ya Ajira Utumishi | Taasisi Mbalimbali PDF 20241115

Hii hapa orodha ya Majina ya Walioitwa Kazini Sekretarieti ya Ajira Utumishi | Taasisi Mbalimbali PDF Tangazo la Matokeo ya Usaili kwa Waombaji Kazi PSRS 2024.

Kuitwa kazini utumishi na ajira portal
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anawaarifu waombaji wa nafasi mbalimbali waliofanya usaili kati ya tarehe 12 Septemba 2024 kuwa matokeo ya usaili yamechapishwa rasmi. Matokeo haya yanajumuisha waombaji waliofaulu pamoja na wale waliokuwa kwenye kanzidata kwa kada mbalimbali na wamepangiwa vituo vya kazi kufuatia nafasi zilizopatikana.

Maagizo kwa Waombaji Waliofaulu Usaili​

Majina ya Walioitwa Kazini Sekretarieti ya Ajira Utumishi | Taasisi Mbalimbali PDF

Waombaji wote waliofanikiwa wanatakiwa kuchukua barua zao za kupangiwa kituo cha kazi ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya tangazo hili. Barua zinapatikana katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) katika majengo ya Dkt. Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi. Barua ambazo hazitachukuliwa ndani ya muda uliowekwa zitatumwa kupitia anuani za posta za wahusika.
Pitia: kuitwa kazini halmashauri ya Wilaya ya Ubungo

Taarifa Muhimu kwa Waombaji Walioitwa​

Kuitwa kazini Sekretarieti ya Ajira Utumishi na Ajira Portal

Waombaji wanaotakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi wanapaswa kufika na vyeti halisi (Original Certificates) vya masomo yao kuanzia kidato cha nne hadi ngazi ya juu. Vyeti hivi vitahakikiwa na mwajiri kabla ya kupewa barua rasmi za ajira. Ni muhimu kwa waombaji kufuata muda uliowekwa kwenye barua hizo ili kuepuka kuchelewa.

Kwa waombaji ambao majina yao hayapo katika orodha hii, tafadhali tambua kuwa hawakufaulu usaili huu. Hata hivyo, mnaweza kujaribu tena nafasi nyingine zitakapotangazwa.
Soma zaidi: Jinsi ya Kujisajili Ajira Portal

Kuhusu Sekretarieti ya Ajira: PSRS ina malengo ya Kufanya mchakato wa kuajiri Watumishi wa Umma kwa kutumia mbinu za kisasa kwa kuzingatia misingi ya usawa, uwazi, na sifa stahiki pamoja na kutoa ushauri kwa waajiri kuhusu masuala yanayohusiana na ajira.
Author
Gift
Downloads
4,060
Views
4,060
First release
Last update

Ratings

0.00 star(s) 0 ratings

More resources from Gift

Latest updates

  1. TANGAZO LA KUITWA KAZINI HALMASHAURI MBALIMBALI 15-11-2024

    Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwataarifu waombaji kazi wa...
Back
Top