Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilitoa taarifa ya kusitishwa usaili wa Walimu tarehe 17 Oktoba, 2024 ambapo taarifa hiyo ilitokana na tangazo la kuitwa kwenye usaili la terehe 15 Oktoba, 2024.
Hivyo, kupitia tangazo hili, Katibu wa Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma anapenda kuwatangazia waombaji kazi wote wa Kada za Ualimu ambao usaili wao ulisitishwa kwa muda kuwa usaili huo utafanyika kuanzia terehe 14 Januari, 2025 mpaka tarehe 24...